Agroecology and Agriculture

Kaunti ya Bungoma ni miongoni mwa zile zilizoorodheshwa katika ukuzaji bora wa kahawa nchini huku ikiwa miongoni mwa kumi bora katika upanzi wa zao hilo.Kaunti ya Bungoma pia imejizatiti Kwa juhudi za kustawisha mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya anga Kwa kuhimiza wakulima kutekeleza mbinu bora katika kilimo chao.Kahawa  ambayo ni kitenga uchumi hasa katika eneo la Mlima Elgon imevutia zaidi ya wakulima wapatao alfu mia tatu huku umuhimu wake ukijidhihirisha wazi kwa wenyeji na mazingira ya eneo hilo kwa ujumla.Mary Wekesa  mmoja wa wakulima wa zao hilo kutoka eneo la Cheptais anasimulia safari yake ya ukulima wa kahawa zao ambalo anaelezea kuwa lina faida si haba.Kahawa hutumika kwa njia mbali mbali ili kustawisha mazingira. Maganda yake hutumika kama mbolea, huku aina hii ya kilimo ikichanganya mbinu za jadi na za kisasa kustawisha rotuba ya udongo na mazingira kama anavyoelezea Pauline Andeso mkulima wa zao hilo kutoka eneo la Malakisi.Naye Jackline Watima mkulima wa kahawa kutoka chesikaki  kwa zaidi ya miaka ishirini. Anawashauri wakulima wenzake kutumia mbolea tofauti kama njia moja ya kuimarisha rutuba katika mchanga. Pia anatoa wito kwa serikali ya kaunti ya Bungoma kusaidia wakulima kupata mifugo haswa Ng’ombe watakao toa mbolea asili ambayo ni bora zaidi kwa mbolea mboji.Jackson Chebusi mtaalam wa zao la kahawa na pia mwenyekiti wa wakulima kule mlima Elgon. Jackson anawashauri wakulima kupanda kahawa pamoja na mimea mingine kama njia ya kukinga zao hilo kutokana na jua hasa hasa katika maeneo yaliyo na joto na kuongeza rotuba kwa udongo.Anashauri wakulima vile vile kuwa makini kutumia mbinu bora wanapopanda kahawa katika maeneo ya miteremko ili kuzuia momonyoko wa udongo.Wakulima wa kisasa wanahimizwa na wataalam kuzingatia kilimo ambacho kinatilia maanani madiliko ya hali ya anga na uhifadhi wa mazingira. Katika hali hii wanahimizwa kuendeleza kilimo kwa ustadi, mchanganyiko wa mazao na mifugo, kubadilisha mazao kwa misimu bila ya kuzingatia zao moja tu ili kuongeza rotuba kwa udongo na kukuza miti. Wakulima wa Kahawa katika eneo la mlima elgon wamekumbatia aina hii ya Kilimo.

2356 232

Suggested Podcasts

Maurice Cherry, Lunch

American Society of Clinical Oncology (ASCO)

Michael Bruce Image Consulting

GreenPath Financial Wellness

John smith