Ep. 46 - Salama Na HK | NJE YA BOX KIDDOGO

Sikuwahi kuujua ufahamu wa Dr Hamisi Kingwangala kwenye suala la dini kwa kiasi ambacho ameniambia wakati tunaongea kwenye kikao chetu hiki, na alinilelezea kwa majina yake ya kizuoni huku akiniambia nini kwa binafsi yake anaweza kukifanya kwa kituo pale anapotaka, lakini pia aliniambia juu ya suala la yeye kutokua anaswali sala tano kama ilivyokua zamani na kwamba si jambo analojivunia asilan! Hii ilikua mara yangu ya pili kukutana na kuongea nae kwa kituo, kama ilivyokua kwa Taji nae pia niliongea naye miaka ya nyuma wakati nafanya Mkasi, na kwa kuongea naye round hii nimejifunza kwamba hawa ni kama watu wawili tofauti kabisa na si kwa ubaya, yule wa kwanza alikua si muongeaji kama huyo wa sasa  kwasababu amekua kwa kiasi flani na kukua ni jambo ambalo sisi wenyewe na wazazi wetu huangalia kwa makini kuanzia pale ulipokua tuseme miaka mitano iliyopita na sasa na mipango na maratajio yako. Kwa hili Sheikh HK kaserebuka nalo vizuri tu. Hakuna mtu asiyemfahamu Hamis Kingwangala ndani ya nchi hii na nje, jinsi ambavyo alifanya kazi nzuri ya kampeni ya kuitangaza Tanzania duniani kwa umaarufu wa vivutio vya utalii wetu na utajiri wa nchi yetu pendwa. Alichukua muda huo pia kutembelea karibu mbuga zote na nchi hii na wakati huo huo kupambana na majangili na waharibifu wa wanyama pori, vita ambayo ilikua ndo stori ya kipindi flani hapo nyuma. Yeye HK alikua anamalizana na maneno ya walimwengu ambao walikua wanaongea mengi kwenye mitandano ni kwa  yeye. kuendelea kupiga  kazi yake vizuri tu mpaka akamaliza miaka mitano ya kwanza ya Rais aliyempa cheo hicho kwa usalama tu, nasema hivyo kwasababu kuna wengi ambao walikua wanateuliwa lakini siku zao za kukaa ofisini hazikua nyingi sana ila HK aliweza kuendana vizuri na mawimbi kwenye bahari ya uongozi ambayo bila ya shaka ilikua na mitihani yake. Pia umaarufu wake mwengine Bwana HK ulikuja baada ya kuwa ntumiaji mzuri sana wa Twitter, sehemu ambayo huitumia kwa kufanyia kazi yake ya kuitangaza nchi na pia kumalizana na ‘wabaya’ wake wote ambao wamekua wakila nae sahani moja kila mara panapokua na jambo ambalo yeye amesema au kuwakilisha mooni yake juu ya suala flani. HK hana tabia ya kuona haya kumjibu mtu ambaye kwa namna moja ama nyengine anakua kamgusa pale alipokua hapataki yeye au pengine tofauti tu ya mawazo, muda mwengine utakuta watu wamefika huko. Kubwa kuliko ilikua hii ya mwaka huu ambayo alihoji juu ya uteuzi wa CEO mpya wa klabu yake pendwa ya Simba na pia suala la mwekezaji kutimiza ahadi yake ya kuipa Simba shilingi bilioni 20 za kuendeleza klabu. Hili suala liliamsha zogo kubwa kati ya HK, muekezaji wa klabu pamoja na mashabiki wa Simba, lilifanya pia tujue siri za ndani za kibiashara kati ya wawili hawa na jinsi ambayo wote wawili walivyokua wanajibizana mitandano ilifanya watu wengi wanyanyue nyusi kwa mshangao na kujuzwa mambo ambayo pengine yalikua hayana faida kwa watu wengine kujua. Hivi karibuni wawili hawa walimaliza tofauti zao huko huko kwenye mitandao hiyo hiyo ya kijamii kama walivyofanya awali. Niloitaka kujua kama kuna muendelezo wa hayo maongezi yao, kama walishakutana toka majibizano yale yatokee, pia tuliongelea ajali ambayo aliipata akiwa kazini na ambayo pia ilizungumziwa na watu wengi. Pia niliongea nae kuhusu Rais Magufuli, uchaguzi wa mwaka huu ambao chama chake kimeshinda  kwa ushindi mnono na jinsi ambavyo hakupata nafasi kwenye baraza la mawaziri na manaibu wake ambalo limeundwa hivi karibuni na ambavyo aliipokea taarifa hiyo. HK ni mtu poa sana, kijana ambaye ni Kiongozi, Baba, Kaka na mfanyabiasha mzuri tu ndo darasa letu la wiki hii na yangu matumaini kana kawaida atakua na jambo la kukufunza kwahiyo tafadhali enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

2356 232

Suggested Podcasts

Poetry Foundation

Cory Gregory a John Fosco

Jae Brooks IG:midnightmastermindmedia

BBC World Service

Issue One