Ep. 45 - Salama Na TAJI | TABASAMU LA SWAHIBA
Pia anafahamkika kama Master T, mwenye sauti yake tamu ya kumfanya mtu abadilishe mawazo na kufanya anachosema yeye, lafdhi nzuri ya maneno ya Kiswahili na Kiingereza na tabasamu zuri kabisa lililokaa mahala pake na hiyo ndo tofauti ya Taji Liundi na watangazaji pamoja na hata viongozi wa department mbali mbali kwenye vyombo vyetu vya habari vya ‘siku hizi’. Taji alibahatika kuzaliwa kwenye familia yenye uwezo kwa kiasi chake na malezi bora aliyapata kwa Baba yake ambaye muda mwingi alikua akisafiri nchi mbalimbali kutokana na kazi yake na hii pia ilimfanya ajengeke kwa kiasi flani, kuweza kujiamini, kuongea lunga zaidi ya moja na mapenzi yake na muziki pia yalianzia hapo. Aliniambia katika maongezi yetu haya kwamba kukaa na Marehemu Mzee wake ambaye alikua busy wakati mwingi ndo ulimpa mwanya wa yeye kujifunza mambo mengi ya nje ikiwa ni pamoja na muziki na michezo kama football na basketball. Pia aliniambia alikua mpigaji simu kwenye radio mzuri sana tu, na kwa kiasi flani hiyo ilifanya mapenzi yake na radio yaanzie na aliporudi nyumbani na familia yake alipata msukumo wa kwenda kutafuta kazi kwenye radio. Kuna tukio pia lilitokea vacati akiwa na umri kama miaka saba au nane ivi, ambalo lilikua linahusiana na wivu wa mapenzi ambao Mama yake alikua nao kwa marehemu Mzee wake na ndo ambalo lilifanya maisha ya Taji yabadilike sana sana. Na hihi simulizi alitupa kwenye kipindi chetu hiki, hii ni tettes ambayo niliiskia mara nyingi tu wakati nakua na kistaarabu kabisa ilibidi nimuulize Kaka yangu kama atakua huru tuizungumzie hapa, na hakua na hiyana kabisa. Tuliongelea jinsi ambavyo Mama yake aliwauwa ndugu zake na jinsi ambavyo yeye aliponea chupuchupum anatuelezea vizuri sana kwenye maogezi yetu haya. Taji pia alikua boss vanga wa kwanza mimi kama Salama, kazi yangu ya kwanza yeye ndo alinipatia nafasi kwa moyo mmoja kabisa, aliniambia nifanye majaribio ya sauti na kusoma habari flani ya Tennis na mengine baada ya hapo ni history kama wazungu wanavyosema. Kwahiyo pia nilimuuliza kiaina ni nini hasa aliona ndani yangu na kama anaikumbuka hiyo siku, maana binafsi nakumbuka mpaka nilichokua nimekivaa Salama mimi. Maneno pekoe hayawezi kusimulia jinsi ninavyo mshukuru kwa kuniamini na nafasi, Mwenyezi Mungu aendelee kumlinda, kumpa afya njema na kumtimizia kila takwa la moyo wake In Shaa Alla. Kwa kumalizia pia mi Kaka yangu tulizungumzia mustakabali wa muziki wetu na wanamuziki wetu, radio na watangazaji wa kisasa na pia muongozo kwenye masuala ya kazi, Taji pia aliniambia naye ameanza kutimiza ndoto zake kidogo kidogo kwa kutoa single yake ambayo hata mimi nilishtuka kidogo kwa furaha baada ya kuona yuko serious, na sio wimbo tu, ni wimbo MZURI. Nilienjoy sana kuongea na Taji kwenye kipindi hiki na zaidi nilifurahi kwasababu anakua anapatikana pale unapomhitaj, hii inakuja hata kwako wewe, kama utakua unahitaji ushauri wa masuala ya kazi na hata maisha, Taji hatokosa la kukuambia ambalo litakufanya ujiskie vizuri, na kuzogeza mambo, hilo nakuahidi. Hii nimeifanya kwaajili yangu na yako na yangu matumaini itakufunza jambo na kukufanya utabasamu. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support