Ep. 44 - Salama Na MWAKINYO | VITASA OVERLOAD
Hassan Mwakinyo kwa Mama yake ni kama ni kama mkate kwa chai tu, lazima ulainike. Sentensi hii imeanzia hapa baada ya kufuatilia kwa makini na kuambiwa hasa ni kitu gani kinachomfanya Champez atake kuwa bora zaidi na zaidi, na kutaka kupata kile anachokipata kwa nguvu zaidi na zaidi kila siku kila asubuhi anapoenda kukimbia, au kila jioni anapokua gym au anapokua ulingoni, na amini kwamba Mama yake ndo anayemfanya atake kuwa bora siku zote ili aweze kumbadilishia maisha yake kwa uzuri. Champez Mwakinyo sio moto pekee kwenye familia yao na Kaka yake mkubwa alianza haya mambo ya ngumi kwanza kwa kujiingiza kwenye kick boxing na akawa sio mkali au hodari vile kama ambavyo Mwakinyo amefikia lakini muongozo wake ndo ulomfanya Champez awe hodari kiasi hiki na kuna mpinzani ambale alikua anamsumbua sana kaka yake ila baada ya miaka kadhaa Mwakinyo alimalizana naye vizuri tu na kuweka heshima kwenye familia. So niliongea na Mwakinyo kuhusu ile fight ambayo ilitufanya sote tumfahamu uzuri, nilitaka kujua alifikaje kule Liverpool na yule mpinzani alimpataje? Vipi na yule jamaa ambaye alibeba headlines zaidi kuliko hata Mwakinyo mwenyewe? Walikutana vipi? Ni kweli alikua anamtaka Kelly Brook? Au yeye mkalimani ndo alikua na ajenda hiyo? Je kuna siku tutaweza kuiona hiyo fight? Mambo mengi yalitokea wakati Mwakinyo akiwa Uingereza, kulikua na suala la kuchukua pesa na kuacha apigwe kulikua na suala la yeye kupotea kabla ya kwenda kupima uzito. Suala la Mama yeke kupata ajali kabla ya yeye hajaenda England na mambo mengine kibao. Alirudi pia nchini na akapata kudhaminiwa na kampuni moja kubwa ya masuala ya betting, huo mkataba uliishaje? Alipata faida yoyote? Hivi karibuni alipigana na Jose Carlos Paz kutoka Argentina ili kuweza kutetea ubingwa wake wa WBF kutoka IBA hapa jijini Dar es Salaam, pambano lilikua la kiwangi cha juu, la kimataifa tuseme lila kwenye suala zima la uandaaji na viingilio kama lilileta utata kwa mashabiki zake. Nilimuuliza Mwakinyo kama kile ndo alichokua anataka maana kwa uelewa wangu, boxing ni mchezo wa watu wa chini hapa nyumbani kwetu, je ilikua sawa kwa yeye kukubali viingilio vile? Au inabidi tukubaliane kwamba enzi zimebadilika na kwamba mambo ndo yaka hivyo now? Nini kinafuata kwake? Nini anataka kwenye maisha yake? Vipi kuhusu mpinzani wa hapa nyumbani ambaye wapenda ngumi wengi ndo wamngependa apigane naye? Maoni yake yepi? Kweli tutaweza kuona hilo pambano? Tulitegemee lini? Jibu lake ndo litakupa muongozo kama tunayoyataka yatakua au la! Yangu matumaini Champez atakufundisha mambo kadhaa kuhusu heshima, mapenzi, malengo, dini na kujiheshimu na jengine lolote ambalo unaweza ukapata humu. Tafadhali enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support