Ep. 43 - Salama Na MANTANA | MIPANGO BAABA

Sniper Mantana si jina lake la Serikali na ukiskiliza kwa makini kwenye maongezi yetu haya utaelewa uzuri kwamba jina hilo alipewa kutokana na umahiri wake wa kulenga pale kwenye malengo yake na kufanikiwa kutokana na juhudi zake ambazo unaziona hata kwa mbali tu na ki ukweli kabisa hiyo ni moja ya sababu kubwa ilonifanya nitake kukaa naye chini ili anifahamishe hasa siri ya mafanikio yake na kile kinachomsukuma kufanya afanyayo. Mara ya kwanza kumsikia Sniper ilikua kutoka kwa AY ambae yeye walikutana huko Malaysia na alikua ni msanii wa kwanza kwenda kutoa burudani huko, Sniper ndo alifanya mipango yote hiyo. Alikua na uwezo wa kuwakusanya wanafunzi wenzake wa ki Tanzania, Kenya na Afrika kwa ujumla na hata wageni wa mziki wetu pamoja na kuwapa burudani kutoka ukanda huu. Alifanikiwa, aliweza kuwa na sehemu ya kupiga disco na concerts na aliweza kusoma na kurudi na digrii yake vizuri tu kabisa. Kampuni yake ya Straight Up Vibes ndo kinara sasa hapa kwetu kwa kufanya kazi nyingi za makampuni na promotion ila pia yeye kama yeye pia ni promoter aliyetulia kabisa, anayejielewa na ambeye pia amefanikiwa vizuri kuliteka soko la muziki hapa nyumbani kwa kuweza kuwaleta wasanii wa nje ambao wameweza vizuri tu kwa kutoa burudani ambayo wanastahili kwa viingilio vikubwa wanavyolipa. Kampuni yake ilifunga mwaka jana kwa concert ya heshima kabisa na mwaka huu ameuanza vizuri tu kwa kuendeleza pale alipoishia. Humu, binafsi nilitaka kujua safari yeke na mambo mengine kama haya lakini pia niliongea nae kuhusu mustakabali wa muziki wetu hapa nyumbani, kwa kirefu tu. Yeye kama promoter amekua akidondosha wasanii wengi hapa ambao wengi wao wamekua wakilipwa mapene mengi na hilo likasababisha baadhi ya wasanii na raia wa kawaida kuuliza maswali juu ya sisi kuendelea kuwatajirisha wenzetu wakati hapa nyumbani yuna vipaji vikubwa ambavyo navyo vilikua vinahitaji kupewa mapene hayo , na kama kuna sehemu wanakosea basi waambiwe ni wapi ili nao watoke! Mantana hakua mchoyo juu ya nini kinatakiwa kufanywa na pia kwamba mlango wake uno wazi kwa yoyote atakayehitaji msaada wa jinsi ya kufanya mambo kadhaa ili vitu viende. Sniper ni MTANZANIA, kijana aliyeenda shule na kumaliza kabisa na kupata cheti chake freshi kabisa. Hakukimbia DARASA, alifanya alichokifanya na kujifunza along the way, elimu ambayo inamfanya atoe ajira hapa nyumbani na kuishi vizuri pia. Nilimleta hapa ili yatu waskie alipotoka na nia na madhumuni yake huko mbeleni na kama vipi uchote mawili matatu ili yaweze kukusaidia hapa na pale. Tafadhali Enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

2356 232

Suggested Podcasts

Rogin Kim

Sakura: Study Japanese Listening with our Announcer from Japan

Lutheran Public Radio