Ep. 42 - Salama Na EDO KUMWEMBE | MWENYE SHOKA HAKOSI KUNI
Edward ‘Edo’ Kumwembe ni rafiki yangu wa si miaka mingi, pengine sita tu toka mara ya kwanza kukutana nae wakati wa uzinduzi wa kampuni moja ya kamari hapa nyumbani. Nakumbuka alikua akimtania sana Fid Q na jinsi ambavyo Fid alikua hamjibu Edo ndo ilikua inachekesha kabisa, wengi wetu tunafahamu Fid ana maneno mengi, ila mbele ya Edo huwa hana hata maneno kabisa. Tulicheka sana, na baada ya hapo tukaanza kufanya kazi pamoja kama Influencers kwenye hiyo kampuni, na baada ya miaka mitatu Allah akabariki nikapata ile kazi ya Super Sport, na kama ulikua hufahamu, Edo ndo alinipigia chepuo nyingi sana ili niweze kuipata hiyo kazi ambayo kiiila ‘mchambuzi’ wa futiboli alikua anaitaka, mpaka baadhi ya wastaafu na viongozi walikua wanaitolea macho, lakini Mungu akanibariki nayo mimi Salama. Yeye pia (hii ilikua siri ????) ndo alikua mtu wa kwanza kuniambia kama mkeka umetiki, tunaenda zetu Johannesburg. Furaha yangu ilikua kubwa sana, na nilikua napiga kelele ndani yangu, ila kwa nje nilikua na play cool, najifanya oh. okay…Habari nzuri hii Edo, asante sana. Kumbe ndani kuna Meja Kunta anaimba singeli kwenye pati ya kitaa, kelele nyingi sana. Mungu si Athumani na safari yangu kwa kwanza ya KIKAZI ilikua ya AFCON2018, unaweza aka guess ni nani nilipangiwa kufanya nae kazi kwenye kuanzia mechi za mtoano mpaka fainali hizo? Ndio umepatia, ni Edo Kumwembe. Alifanya maisha yangu yawe rahisi sana. Alinisaidia sana kunitoa hofu na kunifanya niwe calm na kuweza kuifanya kazi ile kwa uzuri kadri ya uwezo wangu, akiniona tu niko down au siko 100 alikua akiniambia, ‘oya, hii kama ubwabwa tu’. Huo ulikua ni msemo wa Maulid Kitenge ambao Edo aliuleta kwangu akimaanisha hii kazi ni rahisi sana, ni kama kula wali tu ????. Mungu ni mwema. kazi ilienda freshi, Edo alinipa bata la kufa mtu. alinionyesha (na bado anaendelea) kunionyesha Jozi. Ananifundisha mambo mengi kuhusu soka na watu wake na kila kitu chake kila siku, hata kama haniambii mimi ila najifunza tu kutoka kiwale kila siku. So nini hasa ambacho kinamfanya Edo awe ‘mnyama’ kiasi hiki? Well, ndo Mungu alivyo mbariki. Hana kununa wala kulalamika ili mambo yawe magumu, yeye huchukulia vitu kwa wepesi tu na kumalizana navyo vizuri tu. Anafanya anachokitaka kwa wakati wake. Hana majungu, hasemi pembeni yani, kama ana la kukuambia basi jua atafanya hivyo bila ya kukupepesa, kitabia flani ambacho tunafanana kiasi. Urafiki wetu pia unaendana kwa kupenda kucheka, kama nilivyosema awali, ukikaa naye kucheka ni uhakika na hilo pia ni jambo langu pendwa kabisa. Inawezekana ikawa anakusema wewe mwenyewe mpaka inabidi ucheke tu, inawezekana ikawa kuhusu football, au siasa au muziki au maisha, mapenzi yani wewe tu. Kusema za ukweli ni raha tu ukiwa nae. Pia anapenda MAISHA MAZURI na haogopi kuyafanyia kazi ili aishi hivyo. Pia yeye ni moja wa waandishi wa habari wachache sana ambao wanajituma sana, Edo anaweza kuweka hela zake akasafiri tu ili aweze kufanya interview zake na zikawa tofauti kabisa na waandishi wengine. Hii inampa uwanja wa kufanya vizuri zaidi na kupa uhuru wa kuongea anachokijua na sio kuongea tu kutokana na alichosoma kwenye internet. Tulipokutana mezani tuliongea kuhusu yeye kama toto kutoka kwenye familia ambayo haikua vibaya, familia ya kisomi tunaweza kusema. Vipi alianza kufanya anachofanya sasa? Nani alimvutia? Pia kuna mustakabali wa mpira wetu hapa? Simba na Yanga? Ni kweli soka letu limepanda kiwango? Vipi kuhusu wachezaji wetu wanaocheza soka nje ya Tanzania? Chama cha mpira je? Viongozi wake? Mpango wa mbeleni anauonaje? Je, unafahamu kama Edo pia ni muandishi mzuri sana wa makala mbalimbali kwenye gazete la Mwananchi na Mwanaspoti? Maongezi haya yangeweza hata kufika siku ya pili maana mimi na yeye tunaweza kuongea na kucheka for days ndo maana mimi na wenzangu tukaona sio mbaya kukuletea Kaka hapa ili nawe ufaidi na kujifunza kama ambavyo mimi nafanya. Yangu matumaini ata enjoy. Love, Salama --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support