Ep. 40 - Salama Na KADUGUDA | SIMBA WA YUDA

Mara ya kwanza kukutana na Mwina Kaduguda na tukaongea kiasi ilikua kwenye seminar ambayo timu ya Simba ya wanawake ilikua imeandaliwa kwaajili ya kuwaweka sawa kwenye masuala ya biashara, jinsi ya kujitunza wao na vipaji vyao, jinsi ya kuishi na umaarufu na pia kusimamia masuala yao ya kifedha. Mzee Kaduguda alikuwepo kwenye kikao hiko akiwa kama Mwenyekiti wa klabu ya Simba, na pia mmoja wa watoa nasaha kwa mabinti hao. Na kusema za ukweli toka siku hiyo baada ya kumsikiliza akiongea na wachezaji wale pamoja na Mimi ambaye nilikua mgeni tu kwenye seminar ile, nilivutiwa sana na nikasema haitakua vibaya hata kidogo kama nikipata wasaa wa kuzungumza na mtaalam huyu wa Siasa za kambumbu la Tanzania na Afrika kwa ujumla, mwamba ulojaa uerevu wa kusoma kuhusu soka letu lakini zaidi historia ya Simba Sports Club na zahma za hapa na pale pamoja na siku za neema zaidi ambazo zimeshawahi kutokea pale Msimbazi, mtu pekee anayeweza kukukhadithia yote hayo ni Mwina Mohamed Seif Kaduguda. Toka siku ya kwanza alipomuambia Mama yake mzazi ndoto zake na ambae pia alicheka sana, Mwina hakuwahi kurudi nyuma asilan, badala yake alisoma kwa bidii mno mpaka siku alipofika chuo kikuu. Na baada ya hapo pia hakuacha kujiendeleza, aliendelea kwa kusomea leseni kwa kufundisha mpira na hapo ni baada ya kuwa mmoja wa waandishi wa habari za michezo waliobobea kabisa. Alitaka kuwa tofauti na bora kuliko waandishi wengine, na alifanikiwa vizuri tu. Msukumo huo sasa unatoka wapi? Na pale Simba Sports Club aliingiaje? Lini ndo alijua ana mapenzi na club hii na si nyengine? Kuna mtu alikua anamvutia? Alimshawishi? Alishawahi kuichezea? Alishawahi kuwa footballer yeye? Vipi uongozi alifikaje huko? Na ramani ya soka letu je anayo nani? Inasomeka? Kuna kitabu cha historia ya Simba SC toka miaka ya mwanzo kabisa yeye ndo aliandika, je nini kilimpa msukumo? Inasemekana ndo kitabu ambacho kimefanyia research na kuandikwa vizuri zaidi, je kuna ukweli ndani yake? Na kwamba kinauzwa bila ya yeye kupata malipo yoyote? Akiwa kama Mwenyekii wa SSC yeye haswa jukumu lake ni nini? Kuna ukweli wa hizi habari kuhusu tajiri kutoweka hela alizo ahidi? Yeye kama Kiongozi hili analizungumziaje? Mipango kwenda mbele ikoje? Na vipi kuhusu uhusiano wake na Mo Dewji? Na maamuzi ya kuwa CEO wa klabu ni MWANAMKE hayo vipi? Na je alishirikishwa kwenye maamuzi hayo? Enjoy mazungumzo yangu haya na Simba, ingawa alikua mzungukaji kweli kwenye ujibuji wa maswali yangu niseme tu nimemuelewa. Hakuna kitu kinajengwa ki rahisi au kwa siku moja. Simba Kama klabu inabidi ipewe muda na mipango thabiti ili kufika kwenye malengo makuu na Ndugu Mwenyekiti hilo analitambua. Regards, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

2356 232

Suggested Podcasts

Thomas Rosseland Wiborg-Thune

The Daily Beast

Cory Gregory a John Fosco

First Healthcare Compliance

Dallas Wheatley

The French History Podcast

Dan Hanzus and Bob Castrone

Naatak Inc.