Ep. 37 - Salama Na DR MWAKA | BINGWA
Sikuwahi kukutana na Dr Mwaka mimi kabla ya tarehe 26 ya mwezi wa tisa, ila nilishawahi kuongea nae kwa simu mara mbili kabla ya kukutana, hatukuwa marafiki ila maongezi yetu ya mara ya kwanza kwenye simu yalinifanya nijue kwa kiasi yeye ni mtu wa aina gani, na nilivyokutana nae pia iliongeza heshima yangu kwake kwa kazi anayofanya na aina ya mtu yeye alivyo. Nisiseme kwa kupepesa, alini impress na nilijifunza vitu kadhaa kwa muda mchache niliokaa naye na kuongea nae. Alikuja na mkewe kwenye set ya kipindi na alihakikisha mkewe anafika mpaka kwenye ‘kizuizi’ cha mwisho kabisa kabla ya kufika kwenye meza ya mahojiano na pia alihakikisha macho yake na ya mkewe yanagongana kila anakapopenda kufanya hivyo. Wakati mwengine watu hufanya mambo kwaajili ya camera ili wapate kuongelewa, ila kwa wanaopendana kila kitu huwa kinakua wazi, jinsi wanavyoongea, wanavyocheka, wanavyoangaliana na mengineyo imenipa sababu ya mimi kukubali kwamba wawili hawa ni wanapendana kweli. Na tukumbuke kwamba huyo si mke pekee wa Dr JJ Mwaka kama sote tunavyofahamu, ila hakuna ubishi kwamba yeye pia ni mke wake pendwa kabisa. Maongezi yetu yalianzia kwenye asili yake kama kawaida, na aina ya maisha anayoishi sasa. Kama ni kipaji au alienda shuleni kusoma haya anayoyafanya, na suala la yeye kuwa Daktari Bingwa wa nguvu za kiume na mambo ya uzazi wa kina Mama, na kama hizo tu ndo tiba yeye hufanya. Alinza lini? Alirithishwa? Na je wakati mwengine maneno watu wanasema juu yake yanamkera au yanampa motisha ya kufanya zaidi? Unaikumbuka ile skendo ya kutaka kufungiwa ofisi? Aliimalizaje? Na chimbuko lake haswa hiyo story ni wapi? Ilikuaje akachomoka humo? Na Kuna khadithi na mahusiano yake na wake zake? Hana mmoja mwenzangu. Anawezaje kukaa na wote? Alishapitia ndoa ngapi? Je kasomea taaluma yake hii? Biashara ina faida? Je kuhusu skendo ya kutumia magonjwa ya wanawake na kujipatia wake ni kweli? Kusema za ukweli tumeongea sana, na nimejifunza sana kupitia mazungumzo haya na kama ilivyo ada natumai na wewe utaokota mawili matatu na pengine kupata idea ya ajira na kujikwamua kwa hapa na pale. Dr Mwaka pia ni mtu anayependa watu wengine waendelee na aliniambia kama kwa yeye kuja kwenye kipindi kutasaidia hata kwa theluthi tu na kufanya vijana na wengine wajiongeze basi angependa kuja na alifanya hivyo, kwa hilo namshkuru sana. Tafadhali enjoy rafiki. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support