Ep. 36 - Salama Na JOH MAKINI | KIUNGO

Story ya kwanza siku zote itakua ni jinsi ambavyo mimi na Joh Makini tulipokutana mara ya kwanza, nakumbuka vizuuuri sana sana haswa, jinsi alivyokua mwembamba na asiyekua na maneno mengi, ila macho yake, macho yake yalikua kama Askari wa shabaha ambaye akilenga hawezi kukosa, na guess what? Wanasema katika vitu ambavyo havibadiliki kwa binadamu anapokua basi macho ni moja wapo. Macho yake ni yale yale ya sniper, ila kwa sasa ni ya sniper aliye relax ambaye shabaha zake na malengo yake yanaeleweka. Hahitaji kujitambulisha anapokua kwenye mawindo yake. Heshima zangu nyinyi zinaenda kwake, maana kuweza kukaa kwenye chati toka mwaka 2004/05 mpaka leo hii si jambo ambalo kila muwindaji anaweza kufanya. So anawezaje? Kipi haswa kinamsukuma mwenzetu huyu kuweza haswa kuendelea na kuwa relevant kiasi hiki? Mimi nimefahamiana naye zamani tu, hiyo miaka ya mwanzo ya 2000 na maendeleo yake na kazi yake kama nilivyosema inajielezea. So swali ni anawezaje au amewezaje? Jengine unalotakiwa kufahamu ni kwamba Mwamba si muongeaji sana. Yeye vitendo ndo zaidi. Na mashairi yake ya kibabe na style laini na nyeusi ndo inamfanya aendelee na yake. Kuweza kuweka kundi la Weusi pamoja na kuwa na discipline ya kazi nayo vipi? Kufanya kazi na mdogo wake ambae ni msomi na kama mwenye maneno mengi wakati mwengine inakuaje? Na yeye na Lord Eyes na GNako walitoana wapi? Sawa wote wametoka Arusha ila huu muungano ulikua wazo la nani? Je ki biashara inawalipa? Pia tuliongea kuhusu muziki wa sasa, wa ki leo na mbinu ambazo baadhi ya wasanii wanazitumia ili kufikisha ujumbe wao. Mambo yamekua kama mengi ivi, yeye mawazo yake kwenye hizo mbinu ni yepi? Ashawahi kuchanganyikiwa na baadhi ya vitu ambavyo anaviona mtandaoni? Na kama ana wivu? Kuhusu familia pia nlitaka kuchimbachimba kidogo lakini alikua ngumu maana Joh na familia yake huwa anakua mlinzi haswa. Ni mwaka huu ndo ilikua mara ya kwanza kuona anaweka picha za mwanawe King kwenye Instagram yake. Kwa sababu ambazo yeye anazijua ameamua kufanya hivyo, ya nyumbani ni nyumbani na ya sanaa yake ndo yanaenda mitandaoni. Hapo nilimheshimu sana kwa hilo. Hip Hop si muziki wa lele mama, ni aina ya muziki wa majigambo haswa na maneno tu peke yake hayakufanyi uwe bora mbele ya wana hip hop wenzako bali uwezo wa kuyatembea unayo yaongea na kukaa juu siku zote za maisha yako ndo heshima hapo inapopatokana, na naamini kwa Joh, hilo hatuna deni nae, au niseme binafsi, SIMDAI. Haya, kama ilivyo kawaida yetu yangu matumaini utapata mawili matatu hapa ya kujisogeza na maisha yako na mipango endelevu, na pengine jinsi ya kutokata tamaa katika maisha na kuamini ndani ya mipango yako na maendeleo yako ndugu yangu. Tafadhali enjoy pia. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

2356 232

Suggested Podcasts

Jaclyn Mellone, Online Marketing Strategy for Freelancers, Experts, Personal Brands, Entrepreneurs, and Consultants

Ciro Carrillo

Radio Survivor

Paul Bae

Infinite Potential Media, LLC

Website. Contact

Saravanan shanmugam