Ep. 27 - Salama Na SEBA | MKURUGENZI

Sebastian Bigacho Ndege, jina kubwa  nchini kwetu na anajulikana na watu wa aina tofauti tofauti, hiyo ndo tofauti yake yeye na ‘celebrities’ wengine. Ukiachana na kwamba ni Daktari hodari tu na mtangazaji wa radio mahiri kabisa ambale alijenga historia miaka ya nyuma kwa kuwafanya watu wawe huru kuongelea juu ya suala la maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi, Seba (hivyo ndo anavyofahamika zaidi au Dr Seba au hata Jembe ni Jembe) aliweza kuwafanya watu wawe huru kuongelea pia masuala ya magonjwa ya zinaa na unyanyasaji wa kijinsia kwenye kipindi chake cha NJIA PANDA. Kutumia kipindi hiki, aliweza pia kubadilisha maisha ya yatu wengi ambao walikua wanaishi maisha ya ukimya kwenye suala la ugonjwa na unyanyasaji wa kijinsia, kupitia kipindi hake alitoa elimu ya waziwazi kwenye suala la gonjwa la Ukimwi na kuwafanya watu kuuelewa ugonjwa na jinsi ya  kupambana nao na kujikinga pia. Toka alivyokua mwanafunzi Dr Seba alikua mjanja na muerevu, alijifunza mambo mengi kwenye muda wake wa ziada,  na ndo yalimfanya awe mbele ya wenzake wengi. Nafasi za kuelimisha na uongozi zilipokua zinajitokeza Seba alikua wa kwanza kuzipata maana tayari alikua na ufahamu kuliko wenzake wengi. Alikua mwanafunzi wa kupasi daraja la juu na hilo lilitokana na kutokea kwenye familia ya kisomi ambayo iliweka elimu mbele kabla ya mambo mengine. Dr Seba anafanya kazi zaidi ya nne hata alipokuja kwenye maogezi haya ilibidi tumsubiri kwa muda ili amalizie ku edit CV yake ambayo alikua akiituma sehemu ili aweze kupata kazi aliyokua akiifukuzia. Yeye ni Mkurugenzi wa Jembe ni Jembe FM pia ni Mkurugenzi wa Ndege Insurance lakini pia miaka ya nyuma alikua na Band ambayo kusema za ukweli ilitoa ajira kwa vijana wengi na pia kutoa ushindani kwa band nyengine ambazo pia zilikua zinafanya vyema kipindi hicho. So,anawezaji kufanya yote hayo? Kumbuka pia kuna wakati huwa anafanya yale makongamano ya kuhamasisha vijana kwenye mambo mbali mbali na pia ni moja ya vitu anavyoviweza sana ukichukulia kuongea pia ni moja ya vipaji vyake. Anawezaje? Anajipangaje? Bila ya shaka unafahamu pia kama mwaka huu alitangwazwa  kuwa ni mmoja kati ya watu ambao wanamsisamia Harmonize kwenye mziki wake, kitu ambacho kilinyanyua nyusi za baadhi ya watu. Je ana uzoefu huo? Ataweza? Ni mtu sahihi kwa nafasi hiyo? Na kuhusu familia yake je? Ulikua unafahamu kwamba ametokea katika familia ambayo Mungu aliibariki kwa kipato? Pengine mafanikio yalianza kutokea huko? Majibu ya maswali yetu yalipatikana baada ya kuongea nae pale tu alipomaliza kutuma CV yake. Tuliongea kuhusu udaktari, njia panda, familia, biashara, challenges za maisha, ubunifu na of course Harmonize. Yangu matumaini utapata jambo la kujifunza humu na ku enjoy pia. Love, Salama. Follow: Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

2356 232

Suggested Podcasts

Harpreet Sahota

The Complex Trauma Training Center

Surely You Can't Be Serious Productions, LLC

Jimmy Murrill and Carly Ferrari

Pantheon Media

The New York Times

Himanshu Bhalla

Hubhopper