Ep. 22 - Salama Na Isaya | KOMAA NAO
Mimi na Isaya mara ya kwanza tumekutana kwenye set wakati tunatengeneza episode hii ya 22 lakini kabla ya hapo ilikua ni kufahamiana tu kule kwa social media na respect kwa kila mmoja wetu kwa kile ambacho mwenzake anakifanya. Kwahiyo mkutano wetu wa kwanza ulikua ndo wa kwanza kabisa na haikua ngumu kuanzisha maongezi kati yetu. Wakati nishamseti ili aje kwenye meza pia niliwauliza wenzangu tunaofanya hii kazi pamoja, kila mmoja apendekeze jina au majina ya watu ambao wangependa waje kwenye kipindi na kila jina liwe na sababu ya kwanini tumpe nafasi huyo mtu. Basi jina lake pia lilikua ni muongoni mwa majina yaliyotajwa. Unaweza ukaelewa mpaka hapo juu ya impact ya shughuli anazozifanya. Kama Isaya asingeelezea khadithi ya maisha yake toka utotoni basi hata kwa miaka 100 nisingeweza kudhania alipita kwenye mitihani na mazingira magumu toka akiwa mtoto. Wengi wetu tuna historia za makuaji yetu ila ya mwenzetu huyu ina ujasiri na masikitiko mengi yatakayokutaka uhakikishe mwanao hatokaa akue kwenye mazingira hayo. Elimu kuipata ilikua kwa mbinde, kuwaona Baba na Mama yake ilikua mtihani, kuishi kwenye ahadi zilikokua hazitimizwi na mpaka kufikia kuwa machinga akiwa mtoto kwenye mitaa ya katikati ya Jiji la Mwanza. Ila ukimuona leo hii alivyopendeza na suti yake pengine ya Mtani Nyamakababi utamjua? Kiatu chake kinanga’aa na tabasamu na kujiamini kunamfanya afunge madili ya mamilioni ya dola kwenye project zake mbali mbali. Huwezi ukaamini ndo yeye aliyekua anaenda kuchota maji mtoni kwa baiskeli siku nzima wakati nduguze wanaenda shuleni! Isaya alipambana, jarida la Forbes Africa lilimtaja kama ni moja kati ya vijana 30 walio chini ya umri wa miaka 30 ambao watakuja kuleta mabadiliko makubwa kwenye upande wa teknolojia na mpaka sasa yuko njia sahihi ya kulitimiza hilo kwa mujibu wa maongezi yetu haya. Isaya ametimiza miaka 30 mwezi wa kumi mwaka jana. Ukiachana na kigugumizi kikubwa ambacho naamini pia kilichangiwa na hasira nyingi alizokua nazo wakati mdogo na kukua nazo, Isaya ni muongeaji na natumai kwenye hilo utapata jambo la kujifunza na ku enjoy pia. Love, Salama. Follow: Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support