Ep. 6 - Salama Na MxCarter | LENSMAN

LENSMAN Touch yake katika mambo mengi ndo ambayo inamfanya awe tofauti sana na vijana wengine walokuja mjini nae kwa wakati mmoja, uzuri ni kwamba nilikuwepo wakati mabegi (kama yalikuwepo) hata hayajatua uzuri chini ndo hapo nilikutana na Mashala, aka Michael Sylvester ‘Carter’ Mlingwa. Kwanza ilikua kujuana kwa kwenye mitandao tu na hiyo ni khadithi ya siku nyengine. Kwa wanao nifahamu mimi wanajua kama ni ngumu haswa kumuingiza mtu katika maisha yangu, awe karibu yangu, ajue undani wangu ndo maana nina watu wengi ninaofahamiana nao ila wanaonijua ni wachache. Michael ni mmoja ya watu wanaonijua mimi, na naweza kusema nami namjua yeye. Makutano yetu ya kwanza yalikua kwenye kibaraza cha MJ Records pale nje kwa Marco Chali, nakumbuka mpaka alikua kavaa nini, jeans moja kichupa ivi na fulana ya rangi ya udhurungi, mkononi alikua bracelet ya kimasai zile zinazofunika nusu mkono (mawindo ya wazungu yalikua yanahusiana na muonekano ????), chini alikua na raba tu simple na begi lake la mgongoni. Wembamba wake ulikua unamfanya aonekane mrefu na rangi wake ulikua utani na mfano kwa kila mtu tutakayemuona ana rangi inayoshabihana na yake. Michael alikua na yake ya kufanikiwa moyoni toka siku ya kwanza ila kikubwa zaidi ni roho yake nzuri na kutaka kila mtu anayetaka msaada kwake afanikiwe na hata wale ambao hawajui alikua akiwatafuta aongee nao ili awaelekeze jinsi ya kufanya baadhi ya vitu ili wajiongezee kipato, haswa wanamuziki.  Nakumbuka aliponunua gari yake ya kwanza, alikua ananiachia mimi niendelee nalo na mitkasi yangu kisha yeye anapanda bajaji, si mara moja wala mbili, wala tatu, roho ya aina hii bila ya shaka ndo imemfanya awe anazidi kubarikiwa. Kwa kipindi kisichozidi miaka kumi jamaa yangu huyo amepiga hatua kubwa katika maisha pengine kuliko kijana mwengine yoyote ambae mimi nilimuona toka mwanzo akiwa amefika ‘town’.  Kukaa nae kwenye meza halikua jambo la mjadala maana safari yake ya kutoka kushika camera mpaka kuwa kiongozi wa kampuni yake mwenyewe na kuwaajiri vijana wenzake na kuwa partner wangu kwenye biashara hii unayoitizamana nadhani anafaulu kwa alama za juu kabisa.  Hapa tunakugusia maisha yeke ya utotoni, shughuli za Marehemu Mzee wake, kukua katika familia yenye watoto wengi, mahusiano yake na watu wa mjini na jinsi ambayo ameweza kuepuka kifo mara mbili kwa ajali ambazo moja alitakiwa kabisa awemo na pengine saa hii tungekua tunasema mengine. Ila kubwa kuliko ni kusoma njia alizopita ili nawe uweze kujifunza jambo. Tafadhali enjoy.  Love, Salama.  Follow:  Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

2356 232

Suggested Podcasts

Kellogg School of Management

Financial Times

Asia Matters

VAULT Studios

Seeing and Believing

Cricket everywhere

Shivanand Shukla