SE7EP09 - SALAMA NA DAMIAN SOUL | HARIRI…
Damian Soul ni Superstar na siku ambayo sote tutakubaliana na hiyo statement basi tutaanza kufaidi matunda ya kipaji chake kwa uzuri sana, ila mpaka siku hiyo ifike ni wachache tu ambao wanamuelewa kwa upana huo ndio ambao wataendelea kufaidi kipaji chake kwa nafasi yao. Wale watu wa makampunj mbali mbali kwa mfano CocaCola ambao wanakua na events zao za ndani kwaajili ya watu wao na waalikwa wawili watatu huwa wanamfaidi sana kijana huyu hodari wa ki Tanzania. Na Damian kwa ukali wake akipata nafasi kama hiyo huwa hafanyi makosa hata kidogo, huhakikisha anapeleka mziki wote kwao ili wakati mwengine wanapokua na event basi jina lake liwe la kwanza kwenye list ya waburudishaji wao. Mzaliwa wa Dar es Salaam, mtoto wa Sinza kabisa, Damian amezaliwa kwenye familia ya kishua kabisa, jinsi ambavyo unaona anavaa ki nadhifu vile ukiachana na hereni zake, hivyo ndivyo Marehemu Mzee wake alivyokua ananyuka, nadhifu kabisa. Koti imenyooka na ilivaliwa inakaa hasa mahala pake, kiatu inang’aa vizuri baada ya kuipiga kiwi mwenyewe, Damian anakumbuka unadhifu huo na ki uhakika ameurithi na kuuendeleza. Shule kwake ilikua ni kitu tu ambacho ilibidi akifanye kwasababu pengine kila mtu au mtoto kwa matakwa ya wazazi ilibidi afanye hivyo na ili aweze kutoka pale alipokua ilibidi afunge mabegi yake mpaka Kampala nchini Uganda, kama utakumbuka vizuri kuna miaka ya kati ya 2000 hapo ilikua kama ‘fashion’ kwa watoto wa ki Tanzania kwenda kusoma kule, kwa khadithi nyingi nilizo zisikia wengi wao walikua sio waingiaji sana class na badala yake maisha ya ku party na kujitafuta na kujielewa ndo yalikua ki hivyo zaidi. Haikua tofauti pia kwa Damian Soul, Ila yeye sio kwenye ku party ila kwenye kujitafuta na kujua kwamba muziki ndo kitu alitaka kufanya kwa maisha yake yote. Anakumbuka mti ambao alikua anakaa chini yake na ‘kulicharaza’ sana gitaa na kila aliyekua anapita pale habari alikua nayo. Upekee wake wa kuanzia sauti mpaka style yake ya mavazi ndo unaomtofautisha yeye na wengine, ukimuona tu utajua kama ni Star maana jinsi ambavyo anajibeba ni tofauti na watu wengine. Hii pia inasababisha watu kujiuliza maswali kuhusu maisha yake na vitu apendavyo kama mtoto wa kiume. Yeye kwa mujibu wa maongezi haya na mengine ambayo mimi na yeye tushawahi kuwa nayo hayamsumbui kabisa. Anajiheshimu na kujielewa na pia anajua mipaka iko wapi. Na pengine kama binadamu tunatakiwa kuwaacha watu wawe wao, especially kwasababu hayo ni maisha yao, na kwa heshima na taadhima wanajua jinsi ya kujibeba kama binadamu na zaidi kama mTanzania. Anakumbuka jinsi ambavyo alikua Sinza hasa baada ya Baba yake kutangulia mbele ya haki, anasema mtaani palikua pa moto sana kwa kugumbikwa na wimbi la vijana kujihusisha na vitendo vya kihuni na wizi na kujikita kwenye matumizi mazito ya madawa ya kulevya. Anasema yeye alifanikiwa kukimbilia kanisani wakati anasubiria mambo yake mengine ya shule yakae sawa. Kanisani ambako alijifunza mambo ya muziki ikiwa pamoja na kujifunza kupiga instruments, ukiachana na sauti yake ya kipekee, Damian pia ni mpiga gitaa mzuri sana na muandishi hodari pia wa ngoma zake. Mimi ni mmoja wa mashabiki wake na binafsi nilichukua nafasi hii ili tukae chini na tuyajenge kama familia na watu wengine pia wapate nafasi ya kumskiliza na kumuelewa vizuri. Wengi wamekua wakimhukumu kwasababu tu ya muonekano wake na kama Dada na rafiki niliona kuna umuhimu wa sisi kupata nafasi ya kukaa chini na kumfahamu kinaga ubaga. Kama binadamu wote tulivyo, kila mmoja wetu ana mitihani yake ambayo anapitia, mengine mpaka leo inaendelea na mengine ilikua tunafaulu na mengine kufeli, ila kupitia huko ndo ambako kumetufanya tuwe bora na wapya na kujifunza ni jinsi gani mmoja anaweza kutengeneza maisha yake na akawa mfano bora kwa familia na jamii ambayo imemzunguka. Kama mtoto kwa Mama yake na kioo cha jamii, Damian yuko humble sana na wala hana papara kwenye kuhakikisha anafika pale ambapo anapaona kuna kitu cha yeye kuweza kukaa. Mpaka sasa hayuko pabaya hata kidogo maan --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support