SE7EP06 - SALAMA NA MTANI | SO SILKY

Ushawahi kukutana na wale watu ambao wao ni wa pole tu sana na wanajipenda tu sana ila hawana tu muda wa kuringa au kuji mwabafy kwasababu wao wako talented au wana kipawa kutoka kwa Allah na wanajua? Well mi nishawahi kukutana na watu kama hao na mmoja wao ni mgeni wetu RASMI wa wiki hii ya episode ya sita ya SalamaNa msimu huu. Anaongea kwa utaratibu na kujua kile atakacho, anakipataje na akisha kipata atafanya nacho nini. Huyo sasa ndo mwanangu Mtani Nyamakababi, aka Mtani Beskope.

Kijana wa ki Tanzania mwenye kuelewa somo la leo na ukiachana na mitihani ambayo anakua anaipatia na mara nyingi huwa anafaulu kwa masksi za juu sana, kama daraja basi lake huwa ni la kwanza kabisa! Ufahamu wake na kujiongeza kwake kwenye knowledge na udambwi dambwi kwenye yale ayafanyayo kwa hakika ndo kunamfanya awe trend setter na wengine ambao wanafanya kazi kama ambayo yeye anafanya wabakie kumuona kama Role Model, naamini kwa kiasi kikubwa haata yeye bado hajioni kama Role Model maana safari yake ya kufika kule anapo pataka na kupaota ndo kwanza imeanza kustawi.

Miaka 30 ya umri mwaka huu wa 2022 bila ya shaka ni mwaka mkubwa kwake, ukiwa mtoto wa kiume na tegemeo la familia kufikisha miaka 30 ni jambo kubwa, hasa ukiwa hujaoa na una ramani ya maisha kama alo nayo yeye bila ya shaka utakua na mipango mingi, mengine yanawezekana na mengine ni kwa Rehema za Mwenyezi Mungu zaidi. Najua yeye anajua kama Mzee na Mama wanataka kumuona kijana wao akiwaletea wajukuu na I hope wazazi wake hawato subiri kwa kipindi kirefu kama ambacho Mama yangu mimi ameendelea kungoja ????. Yeye tayari yuko kwenye mahusiano ya kueleweka tu na ambayo yanaonekana yanaelekea mahali pazuri kwa mujibu wa maongezi yetu haya.

Kama binadamu wa kawaida of course alishawahi kuumizwa kwa uongo na kutokua na uaminifu kwenye mahusiano ila hilo halikuwahi kumrudisha nyuma kwa kuamini huyo alonaye sasa ni wake na anamfaa sana, anamsaidia sana na anamuongoza sana, vitu kama hivi mmoja huhitaji kuskia, hasa yule ambaye tochi yake imefifia mwanga, mwangaza wa mapenzi. Anamkubali sana yule anaye share nae siri zake na struggle zake na ushindi wake mwingi na hata frustrations zake. Na anajua pia kama kuna kupanda na ku shuka kwenye mahusiano na maisha kwa ujumla.

Kwenye meza yetu kulikua na maongezi kuhusu wazazi wake na principle zao za maisha, mdogo wake… Biashara zake na ushindani, mapenzi na uaminifu. Urafiki, ku shinda na kushindwa na pia maoni yake zaidi kwenye vitu mbali mbali ambavyo vinahusu ambayo anafanya na vile ambavyo amekua akitamani kuvifanya. Wapi anajiona baada ya miaka 5 mengine? Well… Hatukuongelea masuala ya hela maana najua hiyo ingemfanya asiwe huru mbele yetu maana mambo kama hayo yanahitaji mtu ambaye hana noma za hivyo ila kwa Ndugu yangu huyu yeye noma anazo, tena nyingi kwahiyo kistaarabu kabisa nikaona NIMUACHE.

Yangu matumaini utaokota kadhaa humu ambayo yatakupa mafuta ya ZIADA ya kutaka kesho uamke salama na kwenda kuwa BORA zaidi ya JANA kwa lolote ambalo utaamua kufanya na lenye kheri na wewe. Mimi nakutakia BARAK ZOTE kwenye hilo maana mifano hai ya wanao jituma na kufanikiwa ipo. Maana yake ni kwamba, inawezekana. Wewe tu!

Love,

Salama.

--- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

2356 232

Suggested Podcasts

BBC Radio 4

Chris Masterjohn, PhD

Vox Media Podcast Network

Eric Velez

Evergreen Podcasts

Anitra a Paul

Muslim Central

BBC Sounds

Ekta MV