MILA YA NYUMBA MBOKE NA MASAIBU YAKE
Miongoni mwa jamii ya wakuria wanaoishi katika kaunti ya Migori NYUMBA MBOKE ni aina ya ndowa ambapo mwanamke huowa mwanamke mwenzake.Tamaduni hii ambayo imekita mizizi miongoni mwa jamii hii inashutumiwa sana kwa kuchangia kuenea kwa virusi vya ukimwi.Makala haya yanaelezea kwa kina mengi kuhusu mila hii ambayo mara nyingi haizungumziwi hadharani.Katika malkala haya niliongea na waathiriwa wa mila hii potovu, wenye kuieneza na vile vile nikachukuwa maoni ya jamii kwa jumla.